Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la ABNA, vyanzo vya ndani nchini Syria vimeripoti kwamba kikundi kinachohusishwa na kundi la kigaidi la ISIS kililenga moja ya vituo vya ukaguzi vya watu wa utawala wa Julani katika mji wa al-Busaira ulioko katika kitongoji cha mashariki cha Deir ez-Zor.
Shirika la habari la Syria "Al-Akhbariya" pia limeripoti kwamba watu wasiojulikana walimuua mmoja wa watu wa utawala wa Julani karibu na mji wa Tell Abyad ulioko kaskazini mwa Raqqa.
Jana pia, vyanzo vya Syria viliripoti juu ya shambulizi la ISIS dhidi ya vikosi vya usalama vya Syria.
Chanzo cha usalama kiliiambia Televisheni ya Syria: "Kutokana na shambulizi la watu wa ISIS kwenye kituo cha ukaguzi cha al-Sabahiya kwenye lango la magharibi la mji wa Raqqa kaskazini mwa Syria, kiongozi mmoja wa usalama ameuawa na mwingine kujeruhiwa."
Hali hii inatokea wakati ambapo ISIS hapo awali, kwa kutangaza taarifa yenye lugha kali, ililitaja utawala mpya wa Syria kuwa "serikali ya kisekula na iliyoasi" na kusema kwamba vita dhidi yake ni wajibu ili kuitakasa ardhi ya Sham (Levant).
Vyanzo vya ndani nchini Syria vimeripoti shambulizi la watu wanaohusishwa na ISIS dhidi ya kituo cha ukaguzi kinachomilikiwa na utawala wa Julani huko Deir ez-Zor.
Your Comment